Tippo:Simba haikuwa salama kwa Kessy

11May 2016
Lasteck Alfred
Lete Raha
Tippo:Simba haikuwa salama kwa Kessy

KWELI sakata la beki Hassan Kessy na klabu ya Simba linazidi kuibua mapya. Unajua nini? Meneja wa beki huyo, Athumani Tippo amesema kuwa anafuraha kuwa mteja wake ataanza rasmi kuitumikia Yanga msimu ujao baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili utakaoanza mwezi Julai.

Hassan Kessy

Ingawa akadai kuwa ilikuwa ni lazima beki huyo aondoke Simba kwasababu haikuwa sehemu salama kwake kutokana na jinsi walivyokuwa wanakiuka mkataba.

Tippo alisema kuwa Simba ilifeli kutimiza vyema yale yaliyokuwa kwenye mkataba wao na Kessy na kwamba walikuwa wakifanya mambo kinyume bila ya kujali mchezaji huku wakimtuhumu kuwa alikuwa akifanya mambo mabaya.

“Walifeli toka mwanzo, walishindwa wenyewe licha ya kuwa mchezaji alikuwa tayari kuendelea. Kimsingi tumeangalia maendeleo ya mchezaji mwenyewe kwani hata wale waliobaki Simba wakiamua kufunguka maisha magumu wanayoishi unaweza kushangaa.

“Kessy anaweza kuogopa kuzungumza lakini, Simba kuna hali ngumu na ndiyo maana unaweza kusikia wachezaji wamegoma wakishinikiza kulipwa mishahara huku wengine wakililia stahiki nyingine,”alisema.

Habari Kubwa