Samatta asaidia ushindi Genk

09May 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Samatta asaidia ushindi Genk

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza kwa kiwango cha juu usiku wa kuamkia jana timu yake, KRC Genk ikishinda 2-0 dhidi ya Zulte Waregem katika mchezo wa Ligi ya mchujo Ubelgiji kufuzu michuano ya Ulaya.

Mbwana Samatta

Nahodha huyo amecheza kwa dakika zote 90 kwa kiwango cha kumfurahisha yoyote katika mchezo huo wa nyumbani, Uwanja wa Cristal Arena mjini Genk.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo kiungo Mkongo mzaliwa wa Ufaransa, Neeskens Kebano dakika ya 47 na beki Mnigeria, Onyinye Wilfred Ndidi dakika ya 63.

Samatta amefanikiwa kuifuta kadi ya njano aliyopewa mwishoni mwa wiki ilitopita KRC Genk ikifungwa mabao 3-1 na Club Brugge katika mfululizo wa michuano hiyo Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge.

Samatta amefikisha mechi 13 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.

Katike mechi hizo, ambazo sita tu ndiyo ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge mchezo wa kwanza.

Habari Kubwa