Zitto Kabwe aachiwa huru

23Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Zitto Kabwe aachiwa huru

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana ya Polisi ya thamani ya milioni 50 muda huu baada ya kulala mahabusu tokea jana Februari 22 (Alhamisi) usiku mkoani Morogoro.

Hayo yamethibitishwa na wakili wa Zitto, Emmanuel Mvula ambae ndie aliyemdhamini na kusema anatakiwa kuripoti katika kituo kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro siku ya Jumatatu Machi 12, 2018.

Zitto Kabwe akiwa nje ya kituo cha Polisi Morogoro baada ya kuachiwa.

Mbunge Zitto Kabwe alikamatwa na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Morogoro wakati akiwa katika muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 19 akiwa pamoja na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo wa malengo ya kushiriki kazi za maendeleo na kuzungumza na kamati za maendeleo za kata hizo.

Habari Kubwa