Serikali yatoa ufafanuzi ushuru na tozo zilizofutwa

19Jun 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Serikali yatoa ufafanuzi ushuru na tozo zilizofutwa

Licha ya serikali kuahidi kufuta tozo na ushuru unaokusanywa na Halmashauri kwa wafanyabiashara wadogo bado kuna Halmashauri ambazo zinatajwa kuendelea kuwatoza ushuru na kodi hizo.

Akitoa ufafanuzi wa suala hilo Bungeni Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-­TAMISEMI­ Selemani Jaffo amesema serikali imefuta ushuru na tozo zote ambazo zilikuwa zinatozwa kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wasio rasmi na walio katika maeneo yasiyo rasmi kama mama lishe, wauzaji wadogo wa mazao ya kilimo na wenye mitaji chini ya Shilingi Laki­moja.

Kodi nyingine zilizofutwa ni ada za vibali vinavyotolewa na serikali za mitaa zinazotozwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa , OSHA, Zimamoto na Bodi ya wanyama na ada ya makanyagio.

Jaffo amesema kufutwa huko kwa tozo na ushuru hakuwahusu wafanyabiashara za migahawa na maduka na wale ambao wapo katika maeneo yanayotambulika na kwamba serikali kupitia Wizara ya Fedha imejipanga kuhakikisha wanaziba pengo la mapato katika halmashauri litakalotokana na kufutwa kwa ushuru na tozo hizo.

Habari Kubwa