Serikali ya marekani hatarini kuishiwa

22Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Serikali ya marekani hatarini kuishiwa

Kutuhumiana kulianza jana kufuatia Bunge la Senate la hapa Marekani kushindwa kupitisha bajeti mpya na kuzuia kuishiwa kifedha kutakakopelekea kufungwa kwa shuguli nyingi za umma.

Rais Donald Trump.

Muswada wa kuitengea fedha serikali kwa ajili ya wiki zijazo haukupata kura 60 zinazohitajika mpaka kufikia dakika ya mwisho usiku wa kuamkia jana.

Rais Donald Trump aliwatuhumu wabunge wa chama cha Democratic kwa kutanguliza masuala ya kisiasa badala ya maslahi ya watu wa Marekani.

Wabunge wa Democratic wanamlaumu yeye kwa kukataa makubaliano ya mapendekezo ya pamoja.

Majadiliano katika mabunge yote mawili yaliendelea jana, kiongozi wa upande wa Serikali katika Bunge la Senate, Mitch McConnell akisema wangerudi ukumbini jana kujaribu kutatua mkwamo huo.

Mkuu wa Bajeti wa Ikulu ya White House alielezea matumaini yake kuwa muafaka ungepatikana kabla ya siku ya leo kumalizika.Lakini kama itashindikana, mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa umma wanakabiliwa na hatari ya kukosa kazi kufungwa kwa ofisi mwanzoni mwa wiki mpya leo.

Kwa mara ya mwisho serikali ilikosa fedha mwaka 2013, na hali hiyo ilidumu kwa siku 16. 

Habari Kubwa