'Scorpion' afungwa miaka 7 jela faini Mil 30

22Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
'Scorpion' afungwa miaka 7 jela faini Mil 30

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Salum Henjewele maarufu 'Scorpion’ aliyekuwa akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho, kwenda jela miaka saba na kulipa fidia ya shilingi milioni 30 kwa kosa la kujeruhi na wizi.

 

Baada ya mahakama kumkuta na hatia Salum Henjewele na kufungwa miaka saba ikiwa pamoja na kulipa fidia ya milioni 30, Saidi Mrisho ambaye alifanyiwa tukio hilo la kinyama amefunguka na kusema kuwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama hiyo. 

Said Mrisho amesema kuwa mtuhumiwa huyo 'Scorpion' alikuwa anastahili kufungwa maisha jela au yeye angetobolewa macho kwa kuwa yeye saizi anaishi maisha magumu huku akipata tabu kwa kuwa alitobolewa macho na kijana huyo. 

Said Mrisho, mwaka juzi 2016 mwezi Septemba, akiwa maeneo ya Buguruni Kwamnyamani majira ya usiku alivamiwa, akaporwa vitu, akajeruhiwa tumboni na kutobolewa macho yake yote mawili yalipelekea kupatwa na upofu na kutoona kabisaa. 

 

Habari Kubwa