Asilimia 40 wajifungulia  nyumbani, wakunga jadi

23Feb 2018
Happy Severine
Nipashe
Asilimia 40 wajifungulia  nyumbani, wakunga jadi

WAKATI serikali na wadau wa afya wamekuwa wakisisitiza suala ya afya ya uzazi salama na kampeni za kupunguza vifo vya wajawazito na watoto, zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito hujifungulia nyumbani au kwa wakunga wa jadi, imebainika.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Utafiti wa Masuala ya Afya Afrika (Amref)  Tanzania, Dk. Frolence Temu.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Utafiti wa Masuala ya Afya Afrika (Amref)  Tanzania, Dk. Frolence Temu, alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa pozungumza wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari, yaliyofanyika nje ya ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mjini hapa.

Dk. Temu alisema kinamama wengi wamekuwa wakijifungulia nyumbani na kwa wakunga wa jadi kutokana na wao na jamii kwa ujumla  kutokuwa na elimu ya uzazi wa mpango.

Alisema kwa kuliona hilo, shirika lake limeanzisha mradi wa uzazi uzima unaofadhiliwa na Global Affairs Canada na katika mradi huo, Amref  imejikita kuboresha afya ya mama, watoto na afya ya uzazi katika wilaya zote za Mkoa wa Simiyu.

“Kwa kuliona hilo, Amref imeamua kujikita katika masuala ya afya ya uzazi, watoto na vijana ili kuhakikisha wanasaidia kupunguza vifo na kuwezesha huduma hizo kupatikana kwa ukaribu,” alisema.

Naye Meneja wa Mradi  wa Uzazi Uzima,  Eli Msebu, alisema walengwa wakuu wa mradi huo ni watu 683,081 ambao ni wasichana na wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito. 

Msebu  alisema mbali na walengwa hao, pia kuna wanufaika wa moja kwa moja 348,567 ambao ni wasichana na wanawake na kati yao kuna wavulana na wanaume.

Alisema mradi huo ni wa miaka minne na ndani ya miaka hiyo shughuli mbalimbali zitafanyika kama utoaji mafunzo kwa wafanyakazi wa afya, wahudumu wa afya na kinamama wajawazito. 

 

Habari Kubwa