Wawili wafariki mgodini Iringa

Tukio hilo limetokea leo katika kijiji cha Masuluti majira ya saa tano asubuhi.

Akitibitisha tukio hilo Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema tayari miili ya marehemu imetolewa ndani ya mgodi.

Amesema chanzo cha watu hao kupoteza maisha ni kukosa hewa baada ya kuingiza jenereta la kuvuta maji mgodini kwa lengo la kuvuta maji na baada ya kuliwasha walikosa hewa.

Hata hivyo amesema jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.