Mrema: Tusiangaike na mateja, tukamate mapapa

Mrema aliyazungumza hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA radio na kusisitiza, jeshi la polisi linapaswa kuhakikisha wanaowapeleka magereza wawe mapapa wa dawa za kulevya ambao ni chanzo cha mateja nchini.

Alisema kuwa kuwakamata na kuwapeleka Magereza mateja ni sababu moja wapo ya msongamano wa wafungwa pamoja na wanachi kupenda kesi na visasi kwa kushindwa kumalizana mitaani.

"Wananchi wamekuwa sababu ya misongamano magerezani kwani kesi nyingine ni ndogo za kuweza kumalizana nyumbani lakini wanaamua kukomoana kwa kupelekana polisi hadi kufikia kufungana," Alisema Mrema.